Jonah 2:2-6

2 aAkasema:

“Katika shida yangu nalimwita Bwana,
naye akanijibu.
Kutoka kina cha kaburi
Kaburi hapa maana yake ni Kuzimu, kwa Kiebrania ni Sheol.
niliomba msaada,
nawe ukasikiliza kilio changu.
3 cUlinitupa kwenye kilindi,
ndani kabisa ya moyo wa bahari,
mikondo ya maji ilinizunguka,
mawimbi yako yote na viwimbi
vilipita juu yangu.
4 dNikasema, ‘Nimefukuziwa
mbali na uso wako,
hata hivyo nitatazama tena
kuelekea Hekalu lako takatifu.’
5 eMaji yaliyonimeza yalinitisha,
kilindi kilinizunguka;
mwani
Mwani hapa maana yake ni magugu yaotayo kwenye sakafu ya kilindi cha bahari.
ulijisokota kichwani pangu.
6 gNilizama chini sana mpaka pande za mwisho za milima,
makomeo ya hiyo nchi yalinifungia hata milele.
Lakini uliuleta uhai wangu kutoka shimoni,
Ee Bwana Mungu wangu.
Copyright information for SwhNEN